Advertisements

Friday, April 19, 2024

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AHUTUBIA KATIKA JUKWAA LA WAFANYABIASHARA WA TANZANIA NA UTURUKI JIJINI ISTANBUL

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wafanyabiashara na Wawekezaji katika Jukwaa la Wafanyabiashara wa Tanzania na Uturuki lililofanyika Jijini Istanbul tarehe 19 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais wa Uturuki Mhe. Cevdet Yilmaz pamoja na viongozi mbalimbali katika Jukwaa la Wafanyabiashara wa Tanzania na Uturuki lililofanyika Jijini Istanbul tarehe 19 Aprili, 2024.
Makamu wa Rais wa Uturuki Mhe. Cevdet Yilmaz akizungumza katika Jukwaa la Wafanyabiashara wa Tanzania na Uturuki lililofanyika Jijini Istanbul tarehe 19 Aprili, 2024.

WAONGOZA NDEGE KUTOKA MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA YA UGANDA (UCAA) WAHITIMU KATIKA CHA CATC


Mkurugenzi wa Huduma za Uongozaji Ndege, Flora Alphonce akizungumza na wahitimu wa  mahafali ya kozi za mbili za Uongozaji ndege(Area Control Procedural& Area Control Survellance) yaliyofanyika katika chuo Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) 
Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa anga Tanzania (CATC) Aristid Kanje akizungumza jambo pamoja kumkaribisha mgeni rasmi kwa ajili ya kufunga mahafali ya kozi za mbili za Uongozaji ndege(Area Control Procedural& Area Control Survellance) yaliyofanyika katika chuo Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) 
Mkurugenzi wa Huduma za Uongozaji Ndege, Flora Alphonce akiwakabidhi vyeti pamoja na zawadi kwa  wahitimu wa mahafali ya kozi za mbili za Uongozaji ndege(Area Control Procedural& Area Control Survellance) yaliyofanyika katika chuo Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) 

MAKAMU WA PILI WA RAIS ATEMBELEA BANDA LA OFISI YA MAKAMU WA RAIS


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akisikiliza maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Hanifa Selengu wakati Makamu wa Pili wa Rais alipotembelea banda la Ofisi ya Makamu wa Rais wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Biashara Miaka 60 ya Muungano katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo Aprili 19, 2024.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akisikiliza maelezo kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Christina Mndeme kuhusu majukumu yanayotekelezwa na Ofisi hiyo alipotembelea banda la Ofisi ya Makamu wa Rais wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Biashara Miaka 60 ya Muungano katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo Aprili 19, 2024.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akisikiliza maelezo kutoka kwa Ofisa wa Uhamiaji alipotembelea banda la taasisi hiyo ya Muungano wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Biashara Miaka 60 ya Muungano katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo Aprili 19, 2024.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akiwasili katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo Aprili 19, 2024 kwa ajili ya ufunguzi wa Maonesho ya Biashara Miaka 60 ya Muungano. Anayempokea ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis.

MAKAMU WA RAIS AZUNGUMZIA MIAKA 60 YA MUUNGANO


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akifanya mahojiano maalum na Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Gabriel Zakaria kuhusu Miaka 60 ya Muungano, mazungumzo yaliyofanyika katika Makazi ya Makamu wa Rais Jijini Dodoma tarehe 19 Aprili 2024.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ametoa wito watanzania wote hususani vijana kuongeza jitihada katika kufahamu historia ya nchi ili kuhakikisha wanapata uelewa wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati akifanya mahojiano maalum na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kuhusu Miaka 60 ya Muungano, mazungumzo yaliyofanyika katika Makazi ya Makamu wa Rais Jijini Dodoma. Amesema ni muhimu vijana kujifunza kupitia nyaraka, vitabu na kutambua historia ya Muungano na namna serikali zilivyofanya utatuzi wa changamoto mbalimbali kuhakikisha Muungano unadumu.

Makamu wa Rais amesisitiza umuhimu wa kutoa elimu kuhusu Muungano kuanzia ngazi ya shule za msingi. Aidha amesema ni vema kutumia mbinu mbalimbali zinazoendana na vijana katika kutoa elimu hiyo ikiwemo Sanaa kama vile muziki na mitandao ya kijamii kujadili namna ya kujenga na kuimarisha Muungano kwa kujadili kwa hoja bila jazba.

KINANA ASHAURI WATUMISHI, WATAALAMU SERIKALINI WASITOE AHADI BILA MIPANGO

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana ameeleza kuwa, ni vema Watumishi, wataalamu wa serikali kutotoa ahadi ambazo wanajua hazitatekelezeka au utekelezaji wake utachukua muda mrefu kukamilika kwani imekuwa ikikwamisha shughuli za maendeleo na kusababisha malalamiko kwa wananchi.

Kinana meeleza hayo alipokuwa akizungumza na wananchi wa Bunda Mjini wilayani Bunda mkoani Mara baada ya kupokea malalamiko ya wananchi kuwa serikali imewataka wahame katika maeneo yao kupisha ujenzi wa mradi wa maendeleo.
Pia, wananchi hao walionesha kukerwa na kitendo cha maeneo yao kuchukuliwa, nyumba kubomolewa na kupewa sharti la kutoendeleza maeneo hayo likiwemo eneo la Kijiji cha Nyantwale.

"Viongozi wa serikali kabla ya kuwahamisha wananchi ni vema wakaeleza ni lini ahadi hiyo itatekelezwa, kama ni fidia, lini fidia hiyo itatolewa, kama ni watu kuhama watahama lini, kama watu ni kupewa fidia watapewa lini," amesema.

Aliongeza kuwa, hakuna sababu ya kutoa ahadi ambayo inachukua miaka mingi kutekelezwa na kila kiongozi anayekuja anatoa ahadi anaondoka.

RAIS SAMIA NA MWENYEJI WAKE RAIS ERDOGAN WA UTURUKI WASHUHUDIA MIKATABA IKISAINIWA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Rais Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais Recep Tayyip ErdoÄŸan wakishuhudia Waziri wa Mambo ya Nje Mhe. January Makamba na Rais wa Baraza la Elimu wa Uturuki Dkt. Erol Ozvar wakitia saini Makubaliano ya Ushirikiano katika Nyanja ya Elimu ya Juu baina ya nchi hizo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais Recep Tayyip Erdoğan katika picha ya pamoja na mwakilishi wa Tanzania ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji TIC Bw. Gilead Teri na mwakilishi wa Uturuki ambaye ni Makamu wa Rais wa Ofisi ya Rais Uwekezaji ya Jamhuri ya Uturuki Zeynel Kilınç, mara baada ya utiaji saini Hati za makubaliano baina ya mataifa hayo mawili tarehe 18 Aprili, 2024
Rais Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais Recep Tayyip ErdoÄŸan wakati wakishuhudia Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Zanzibar Lela Muhamed Mussa pamoja na Rais wa Baraza la Utalii la Uturuki Abdullah Eren wakisaini hati za makubaliano kwa ajili ya kuanzisha ufadhili kwa wanafunzi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Uturuki wanaohitimu katika Elimu ya Juu tarehe 18 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa Ziara yake Rasmi katika Ikulu Kulliye Ankara nchini Uturuki tarehe 18 Aprili, 2024.

MZEE OMAR MUSSA SEIF MKAAZI WA CHOKE DONGO AOMBA KUZUNGUMZA NA RAIS WA ZANZIBAR DK HUSSEIN MWINYI


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakimsalimia na Mzee Omar Seif Mussa Mkaazi wa Donge Choke Mkoa wa Kaskazini Unguja,baada ya kumaliza kwa hafla ya Ufunguzi wa jengo jipya la Skuli ya Msingi ya Hamid Ameir Donge, uzinduzi huo uliofanyika

MAMA, MTOTO WAKATWA MAPANGA NA MUME ALIYELEWA


Mwanamke anayefahamika kwa jina Rhobi Mwita Nkori mkazi wa Serengeti mkoani Mara amenusurika kuuawa kwa kukatwa mapanga na mume wake ambaye alidaiwa kurudi nyumbani akiwa amelewa na kuanza kufanya vurugu.

EATV imezungumza na Rhobi Mwita Nkori ambaye, mwathirika wa tukio hilo ambaye amesema kuwa mume wake anayefahamika kama Wansato Marwa alirudi nyumbani akiwa amelewa na kuchukua panga na kuanza kumkata sehemu mbalimbali za mwili wake na alivyofanikiwa kumtoroka ndipo akamkata panga mwanae wa kike mwenye umri wa miaka 10 katika sehemu ya kichwa.

Naye, msamaria mwema aliyempokea mwanamke huyo baada ya kufika wilayani Tarime, Suzana Mkami Marwa ameleza kuwa mwanamke huyo alifika nyumbani kwake akiwa na watoto 6 mmoja akiwa amekatwa mapanga pamoja na mama yake huku akiiomba serikali kumchukulia hatua kali za kisheria aliyehusika na tukio hilo.


CHANZO - EATV

WIZARA YA MAMBO YA NJE YAJIVUNIA KUIMARIKA KWA DIPLOMASIA, MIAKA 60 YA MUUNGANO



Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) akiongea na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya Miaka 60 Muungano wa Tanzania katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma.

Waandishi wa Habari wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) alipokuwa akiongea nao kuhusu mafanikio ya Miaka 60 Muungano wa Tanzania katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) akisisitiza jambo wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya Miaka 60 Muungano wa Tanzania katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma.

Waandishi wa Habari wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) hayupo pichani alipokuwa akiongea nao kuhusu mafanikio ya Miaka 60 Muungano wa Tanzania katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma.

RAIS SAMIA AKUTANA NA MWENYEJI WAKE RAIS RECEP TAYYIP ERDOGAN WA UTURUKI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Mwenyeji wake Rais wa Uturuki Mhe. Recep Tayyip ErdoÄŸan kabla ya kuanza mazungumzo katika Ikulu ya Kulliye Ankara nchini Uturuki tarehe 18 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwenyeji wake Rais wa Uturuki Mhe. Recep Tayyip ErdoÄŸan mara baada ya kukagua Gwaride la Heshima katika viwanja vya Ikulu ya Kulliye Ankara nchini Uturuki tarehe 18 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride la Heshima mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu ya Kulliye Ankara nchini Uturuki tarehe 18 Aprili, 2024. Kushoto ni Mwenyeji wake Rais wa Uturuki Mhe. Recep Tayyip ErdoÄŸan.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride la Heshima mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu ya Kulliye Ankara nchini Uturuki tarehe 18 Aprili, 2024. Kushoto ni Mwenyeji wake Rais wa Uturuki Mhe. Recep Tayyip ErdoÄŸan.

WAZIRI MKUU MHE.MAJALIWA AFUNGUA SEMINA YA WAKUU WA MIKOA KUHUSU DIRA YA MAENDELEO 2050


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi alipowasili kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma kufungua Semina ya Wakuu wa Mikoa kuhusu Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Semina ya Wakuu wa Mikoa kuhusu Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma
Baadhi ya Wakuu wa Mikoa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipofungua Semina ya Wakuu wa Mikoa kuhusu Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.
Baadhi ya Wakuu wa Mikoa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipofungua Semina ya Wakuu wa Mikoa kuhusu Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Aprili 17, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

SERIKALI KUENDELEA KUDHIBITI ATHARI ZA MICHEZO YA KUBAHATISHA


Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), akijibu swali bungeni jijini Dodoma.

Na Farida Ramadhani, WF – Dodoma.
Serikali kupitia Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini inaendelea kutekeleza mikakati mbalimbali ya kuzuia na kudhibiti athari za michezo ya kubahatisha ili kuhakikisha jamii inakuwa salama.

Hayo yameelezwa Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mlola, Mhe. Abdallah Shangazi aliyetaka kuwajua iwapo Serikali inatambua athari hasi kwa Jamii ya Watanzania zinazotokana na ongezeko kubwa la michezo ya kubahatisha.

Mhe. Chande alisema kuwa kwa mujibu wa Kifungu cha 7(2)(i) cha Sheria ya Michezo ya Kubahatisha, Sura 41, mamlaka ya udhibiti ina jukumu la kuhakikisha kuwa jamii inalindwa ipasavyo dhidi ya athari hasi za michezo ya kubahatisha.

“Katika kutekeleza jukumu hilo, Bodi ya Michezo ya Kubahatisha imekuwa ikitekeleza mikakati mbalimbali ya kuzuia na kudhibiti athari hasi zitokanazo na uwepo wa michezo ya kubahatisha, mikakati hiyo ni pamoja na kuimarisha udhibiti na uratibu wa sekta kwa kufanya ukaguzi wa mara kwa mara na matumizi ya mifumo ya TEHAMA,’’alisema Mhe. Chande.

Thursday, April 18, 2024

WAZIRI JAFO AFUNGUA MILANGO KWA WADAU WA MAZINGIRA


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza wakati wa kikao na ujumbe kutoka mashirika ya kimataifa yasiyo ya kiserikali ya The Pew Charitable Trusts (PEW) na Wetlands International (WI) kwa lengo la kuainisha fursa zilizolopo kwenye uhifadhi wa maeneo ya fukwe, Aprili 17, 2024 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Shirika la The Pew Charitable Trusts (PEW) Bw. Simon Reddy akifafanua jambo wakati wa kikao na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo Aprili 17, 2024 jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amesema Serikali itaendelea kufungua milango kwa wadau wenye nia ya kuchangia katika hifadhi endelevu ya mazingira.

Amesema hayo wakati wa kikao na ujumbe kutoka mashirika ya kimataifa yasiyo ya kiserikali ya The Pew Charitable Trusts (PEW) na Wetlands International (WI) kwa lengo la kuainisha fursa zilizopo kwenye uhifadhi wa maeneo ya fukwe, Aprili 17, 2024 jijini Dodoma.

RAIS SAMIA ATUNUKIWA UDAKTARI WA HESHIMA NA CHUO KIKUU CHA ANKARA UTURUKI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari (Honoris Causa) ya Uchumi kutoka kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ankara nchini Uturuki Profesa Necdet Unuvar kwenye hafla iliyofanyika Chuoni hapo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari (Honoris Causa) ya Uchumi kutoka kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ankara nchini Uturuki Profesa Necdet Unuvar kwenye hafla iliyofanyika Chuoni hapo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari (Honoris Causa) ya Uchumi kutoka kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ankara nchini Uturuki Profesa Necdet Unuvar kwenye hafla iliyofanyika Chuoni hapo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wageni mbalimbali, viongozi na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ankara, mara baada ya kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari (Honoris Causa) ya Uchumi kutoka kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ankara nchini Uturuki Profesa Necdet Unuvar kwenye hafla iliyofanyika Chuoni hapo tarehe 18 Aprili, 2024.

NCHI ZA SADC ZAMPONGEZA RAIS SAMIA KWA MAONO YAKE KATIKA USIMAMIZI WA MISITU YA MIOMBO


Rais wa Jamhuri ya Watu wa Msumbiji, Mhe.Filipe Jaciton Nyusi akizungumza katika Mkutano wa Kimataifa kuhusu usimamizi endelevu wa misitu ya miombo jijini Washington DC nchini Marekani leo Aprili 18,2024.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akizungumza katika Mkutano wa Kimataifa kuhusu usimamizi endelevu wa misitu ya miombo jijini Washington DC nchini Marekani leo Aprili 18,2024.
Rais wa Jamhuri ya Watu wa Msumbiji, Mhe. Filipe Jaciton Nyusi (katikati) akifuatilia mawasilisho kuhusu misitu ya miombo kutoka kwa wawakilishi wa nchi za SADC katika Mkutano wa Kimataifa kuhusu usimamizi endelevu wa misitu ya miombo jijini Washington DC nchini Marekani leo Aprili 18,2024. Kushoto kwake ni Waziri wa Ardhi na Mazingira wa Msumbiji, Mhe.Ivete Maibaze na Balozi wa Umoja wa Afrika nchini Marekani, Mhe. Hilda Suka-Mafdze (kulia)
Baadhi ya washiriki wa mkutano kutoka nchi mbalimbali wakipiga makofi baada ya kikundi cha burudani cha ngoma za asili kutumbuiza katika Mkutano wa Kimataifa kuhusu usimamizi endelevu wa misitu ya miombo uliofanyika jijini Washington DC nchini Marekani leo Aprili 18,2024.